Saturday, October 4, 2008

this from Simon Martha Mkina:


Dear all Hope you are doing fine. I am ok.

Iam just informing you that I have been nominated a journalist of the year in Tanzania 2008 (in investigative journalism). Given a certificate and some money. Nomination was done by Media Institute of Southern Africa (Misa), USAID, Pact Tanzania and a number of journalism guru in the country.

Thanks for your cooperation.

--
Simon Martha Mkina,
Editor/Columnist/Author
Dar es Salaam
TANZANIA


0000000000000


KAMANDA WA ZAMANI WA JESHI LA RWANDA KUANZA KUJITETEA MWENYEWE JUMATATU IJAYO



Na Nicodemus Ikonko, Hirondelle,Arusha



Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Usalama Jeshini nchini Rwanda , Meja Francois-Xavier Nzuwonemeye anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kimbari katika kesi moja na maafisa wenzake watatu, Jumatatu ijayo atapanda kizimbani kuanza kujitetea mwenyewe mbele ya Mahakama ya Umoja wa Mataifa.



Mashahidi 27 wameshatoa ushahidi wa kumtetea mtuhumiwa huyo wa tatu. Wengine katika kesi hiyo ni pamoja na Makamu wake, Kapteni Innocent Sagahutu atakayefuata katika utetezi baada ya bosi wake kuhitimisha ushahidi wake.



Watuhumiwa wengine wawili ambao tayari wameshatoa utetezi wao mahakamani ni pamoja na aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Rwanda , Jenerali Augustin Bizimungu na Mnadhimu mwingine wa Jeshi la Polisi, Jenerali Augustin Ndindiliyimana.



Kwa mujibu wa Wakili Kiongozi wa mtuhumiwa Nzuwonemeye, Charles Taku kutoka Cameroon , kuna uwezekano wa kuitwa kwa mashahidi zaidi katika kesi hiyo wakiwemo wawili ambao tayari wameshaandaliwa wanaotambulika kwa majina bandia ya ‘FK’ na ‘B2’ kwa ajili ya usalama wao.



Mahakama namba II inayosikiliza kesi hiyo Septemba 22, 2008 ilitoa onyo kwa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama hiyo, Hassan Bubakar kwa kushindwa kuwapatia mawakili wa utetezi katika kesi hiyo baadhi ya nyaraka za ushahidi wa maandishi kama inavyotakiwa katika sheria iliyoanzisha mahakama hiyo.



Kwa mujibu wa Wakili Taku, tayari mwendesha mashtaka huyo ameshawapatia nyaraka tatu za ushahidi wa maandishi mawakili wa timu za utetezi kutoka katika majalada ya Kundi la zamani la Waasi nchini Rwanda (RPF).



Kesi hiyo ilianza kuunguruma mahakamani tangu Septemba, 2004



0000000000000000

Kuwe makini na Mitandao- Wanafunzi waambiwa

NA SOLOMON MWANSELE,MBEYA.

WAHITIMU wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ST.Mar's Mbeya, wametakiwa kuzitumia Intaneti kwa kujisomea zaidi, badala kuangalia picha ambazo hazina maadili mazuri kwa jamii.

Imeelezwa kuwa wanafunzi wengi hivi sasa wamekuwa na tabia ya kutumia muda mwingi intaneti wakiangalia picha hizo, hali inayochangia kuwapotosha maadili.

Changamoto hiyo imetolewa na Ofisa Tawala wa shule hizo mkoani hapa, Anuciatha Ngonyani, wakati wa mahafali ya kwanza ya kidato cha nne yaliyofanyika shuleni hapo.

Jumla ya wahitimu 48 wakiwemo wavulana tisa, walitunukiwa vyeti vyao vya kuhitimu na Ofisa Afya wa halmashauri ya jiji la Mbeya Dk.Mathias Kapizo.

Ngonyani alisema wakiwa shuleni hapo wahitimu hao wamefundishwa pia maadili mema na hivyo kuwataka kutojiingiza katika makundi ya utumiaji wa dawa za kulevya na uhuni, kwani watakuwa mfano mbaya katika jamii.

Alisema wanakwenda kwenye ulimwengu wa utandawazi ambao hivi sasa dunia ni sawa na kijiji kimoja, hivyo kuhakikisha kuwa wanajiendeleza zaidi na siyo kuishia kidato cha nne.

"Tumieni elimu mliyoipata mkiwa hapa shuleni kwa miaka minne kwa kujiendeleza zaidi kielimu huko muendako...Msipende kuzitumia Intaneti kwa kuangalia picha za ngono bali kujisomea zaidi" alisema.

Naye mgeni rasmi Dk.Kapizo alisema wahitimu hao wanatakiwa kuwa kioo kwa vijana wengine ambao hawajaweza kupata elimu kama waliyoipata yao licha ya kuwa nao wanatakiwa kujiendeleza zaidi.

Dk.Kapizo alisema:"Nidhamu ni kitu cha kwanza , pili mnatakiwa kuondoa hofu mtakapoingia chumba cha mtihani kwani mtakutana na yale yale mliyofundishwa na walimu wenu hapa shuleni".

Aliongeza kuwa hakuna mitihani inayotungwa nje ya silabasi, lakini wengi wao huwa wanafeli kutokana na kuwa na uoga wanapoingia katika chumba cha mtihani hali inayopelekea washindwe kufanya vizuri mitihani.

Kwa upande wao wahitimu hao wakisoma risala yao kwa mgeni rasmi, waliiomba serikali kutoa ruzuku kwa shule za binafsi katika baadhi ya vifaa kama vitabu na vifaa vingine vya maabara.

Walisema endapo serikali itafanya hivyo, itatoa changamoto kubwa kwa baadhi ya wanafunzi kusomamasomo ya sayansi hivyo kuongeza idadi ya wataalamu katika sekta ya afya na nyinginezo zinazotokana na masomo hayo.


0000000000000


No comments: