Saturday, November 22, 2008

vituko vya Michael Jackson sasa awa muislamu anaitwa Michaeel






Licha ya kushitakiwa na Sheikh Michael Jackson asilimi

Ikiwa ni siku chache kabla ya kutinga mahakamani nchini Uingereza kujibu kesi ya madai ya dola za Marekani milioni saba anazodaiwa kukopa kutoka kwa Sheikh wa Abdullah wa Bahrain, mfalme huyo muziki wa pop duniani ameamua kusilimu na kuitwa Michaeel, walpendekeza jina la Mustafa akalikataa.

Pamoja na uamuzi huo huko nyuma kuliwahi kutokea uvumi kwamba amesilimu na anaitwa Abubakar lakini aliyesilimu alikuwa kaka yake Germain aliyesilimu miaka 1990. pamoja na kwamba kaka yake ndiye anaelezwa kumshawishi asilimi, lakini taarifa zingine wanamuziki wenzake waliosilimu na ambao walikuwepo wakati akisilimu kuwa ni Yousef Islam, ambaye alikuwa akiitwa Cat Stevens, Dawud Wharnsby Ali ambaye awali walikuwa akiitwa David na Idris Phillips.

Michael Jackson alipokuwa Bahrain kwa mshikaji wake Sheikh Abdullah aliahidi kujenga msikiti wenye thamani kubwa. Hata hivyo mwanamuziki huyo mwingi wa vituko alipokuwa Dubai aliwahi kukutwa kwenye choo cha wanawake akijipodoa na kuzusha tflan kubwa.

Habari zaidi ya mwanamuziki huyu mpya soma http://shija.blog.co.in

No comments: