Thursday, October 30, 2008

Uchaguzi wa Marekani unafanyika kwa mfumo wa ‘Electoral College Votes’


Kwa maana Majimbo yote yemepewa idadi tofauti tofauti ya kura kutokana na uwakilishi wake kwenye bunge la Congress. Mfumo huu wa upigaji kura za rais ni wa siku nyingi toka ulianza toka mwaka 1800.

Kura za majimbo ni California lina kura 55, Arizona 10. Maryland 10.nk.Ukijulimsha kura zote hizi ni lazima ziwe zimefika 270 au zaidi. Ili uweze kupata kura hizo ktk jimbo lolote ni lazima umzidi mshindani wako katika majumlisho ya kura zote zilizopigwa na wananchi wa jimbo hilo.

Ukiibuka kidedea kwa wingi wa kura walizokupigia wananchi na ukamzidi mshindani wako ktk jimbo hilo basi mtu wangu unajizolea KURA ZA URAIS katika jimbo hilo (Electoral College Vote).

Inategemea sasa hilo jimbo linakura 3,4 au 7 au 30 za Urais. Yaani kama umeshinda New York, Kura zao za uraisi ni 31, hivyo unazichukua hizo 31 na unaendelea na hesabu za jimbo lingine uliyoshinda.Ukibahatika umetimiza 270 au zaidi basi wewe ni Rais wa Marekani.

Chama cha Democrat majimbo yao wanayoshinda wanayaiita = Majimbo ya buluuu (Blue States)Chama cha Republican majimbo yao wanayoshinda wanayaiita = Majimbo yamekundu (Red States)

Unaweza kuona majimbo ya bluu hapa;

http://www.realclearpolitics.com/

epolls/maps/obama_vs_mccain/

pia unaweza kupata mambo zaidi hapa

http://www.archives.gov/federal-register

/electoral-college/calculator.html

Majimbo ambayo bado hayajaamua kumpa nani kura, yanaitwa SWING STATES.

http://www.politico.com/convention/swingstate.html

000

What is the meaning of Electoral College Vote

A mechanism for the indirect election of public officials. For the purpose of electing the President and Vice President of the United States a 538-member Electoral College is created with each state having as many electors as it has representatives and senators in the national legislature, plus 3 for the District of Columbia. To be elected, a candidate must obtain an absolute majority in the Electoral College, currently 270. If no candidate gains an absolute majority the US House of Representatives makes the choice, with the delegation from each state having one vote.

Most of these arrangements were devised in the Constitutional Convention of 1787 as a compromise between those who proposed a direct popular election of the President and those who preferred to make him subject to election by the legislature. As originally conceived, members of the Electoral College were expected to be prominent state worthies impervious to transient public moods. However, such notions were quickly overtaken by the emergence of parties and the popular election of electors in place of their appointment by state legislatures. The ‘winner takes all’ rule, or convention, that all of a state's Electoral College votes go to the candidate which wins the highest popular vote, is not in the US Constitution; two states (Maine and Nebraska) assign their electoral votes in proportion to the state vote for each candidate. Occasionally, states elect unpledged electors, or electors break their pledge and vote for a candidate other than the one they said they would. Because of the constitutional origins of the college, electors cannot be punished for this.

Reformers regularly query the merits of the Electoral College system for ‘misfired’ elections (where a loser gains more popular votes than the winner) and for the contingency arrangements that come into play when no candidate wins a majority in the Electoral College. The elections of 1824, 1876, 1888, and 2000 misfired and misfires came perilously close in 1844, 1880, 1884, 1960, and 1968. Of these, 1876 and 2000 sparked legitimacy crises. That of 1876 was resolved by a ‘corrupt bargain’ whereby the Republicans kept the Presidency and the Democrats were allowed back into power in the South, where they resumed their oppression of African-Americans. That of 2000 was suddenly ended by the terrorist attacks of September 2001, which conferred legitimacy on President George Bush that his election by one vote in the Supreme Court had failed to do. If all states followed Maine and Nebraska and allocated electoral college votes in proportion to the popular vote in the state, misfires like 2000 would be less likely and misdemeanours in counting (such as those in Florida in 2000) less momentous.

When an election is thrown into the House the bargaining required to form a majority could also create a crisis of legitimacy. This occurred 1800 and 1824 and might have happened in 1960, 1968, 1980, 1992, and 2000. There could also be a dangerous period of uncertainty in that the House would not make its decision until early January, a mere two weeks before the inauguration.

funga mwaka ya wakenya na udugu wa gundi kwa obama


Obama akishinda atalifikia vipi boma?

wabunge wataka uwanja wa kisasa kwa Air Force One, mpya hii!

Wengi wanatazamia huenda Obama akawa akiitembelea Kenya mara kwa mara akiwa Rais wa Marekani

Wabunge wa nchini Kenya wametoa mwito wa kufanyiwa ukarabati haraka uwanja wa ndege wa Kisumu, ili ikiwa Barack Obama atashinda uchaguzi wa rais nchini Marekani, ataweza kuitembelea nchi hiyo kwa urahisi, ambayo ni nchi ya asili ya babake.
Wabunge wa jimbo la Nyanza huko magharibi mwa Kenya wanataka uwanja wa ndege mjini Kisumu upanuuliwe ili ndege ya rais wa Marekani iweze kutua hapo.

Babake Barack Obama ni kutoka katika kijiji kilicho karibu na hapo.

Ijapokuwa Barack Obama hajawahi kuishi Kenya, lakini ameshatembelea nchi hiyo mara tatu.

Waziri wa usafiri wa Kenya, Bw Chirau Ali Mwakwere amesema mpango wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kisumu hautamalizika hadi Julai mwaka 2010.

Wednesday, October 29, 2008

urais na umiss- Sarah Palin




Mgombea mwenza wa John McCain, Sarah Palin katika uchaguzi wa Marekani mwanzoni mwa mwezi ujao anazidi kukumbwa na misukosuko, mara umiss Alaska mwaka 1984, mara kutumia madaraka vibaya kwa kumfukuza kazi shemeji yake, mara hawajai kusoma magazeti kwa muda mrefu na sasa kaingia ugomvi na Rais Hugo Chavez ambaye hata hivyo amesema hajui asemalo anapaswa kusamehewa.

kwa habari zaidi soma hapa; http://shija.blog.co.in/

mfalme wa Nepal akitakiwa umeme kwa madeni



mfalme wa zamani wa Nepal Gyanendra anadaiwa zaidi ya dola za marekani milioni moja (zaidi ya shilingi bilioni moja za Tanzania) na amepewa siku 15 awe amelipa deni hilo la sivyo cha moto atakiona. ukiondoka madarakani mambo ya kunyenyekewa hakuna tena ni undava-undava tu.

kwa habari zaidi fungua hapa: http://shija.blog.co.in/

utani kwa 'Mungu' atimuliwa Dubai



mmiliki wa radio binfasi revin john raia wa marekani ametimuliwa Dubai baada ya radio yake kuingiza utani wa 'Mungu' kwenye kipindi chake cha comedy kwa kuigiza sauti ya 'mungu' wakidai wanaongea naye kwa simu. utani wowote wa Mungu au Mtume Muhammad ni marufuku Dubai.

Kwa habari zaidi fungua hapa: http://shija.blog.co.in/

Ban Ki-moon awaasa waandishi wa habari


Na Maura Mwingira,New York-Marekani

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki Moon, ametoa wito kwa waandishi wa habari duniani kote, kuandika habari zinazowahusu watu wanyonge, masikini na wasio kuwa na sauti, licha ya mazingira magumu na vikwazo mbalimbali wanavyokumbana navyo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Alisema UN inatambua mazingira magumu wanayofanyia kazi waandishi wa habari, na amewataka kutokata tamaa.

Mbali na hilo alisisitiza kuwa Umoja wa Mataifa daima utapinga na kukemea vitendo vyovyote vinavyolenga kuathiri utendaji kazi wao.

Katibu Mkuu alitoa wito huo wakati wa chakula maalumu kilichoandaliwa kwa heshima ya waandishi wa habari wanne, ambao wamefadhiliwa na taasisi ya Dag Hammarskjold, kuja Umoja wa Mataifa, kujifunza na kuandika habari za umoja huo.

Miongoni mwa waandishi hao ni Erick Kabendera kutoka Tanzania anayeandikia gazeti la The Citizen. Kabendera anakuwa mwandishi wa tatu kutoka Tanzania kupata ufadhili wa taasisi hiyo, ikiwa ni miaka zaidi ya 20 tangu mwandishi wa mwisho kutoka Tanzania kufanikiwa kupata ufadhili wa taasisi hiyo.

Mwandishi Mwandamizi wa Magazeti ya Serikali (Daily News) Mkumbwa Ali, ni mmoja wa waandishi waliowahi kufanikiwa kupata ufadhili wa taasisi hiyo.

Jumla wa waandishi wa habari 200 walishindania nafasi nne ambapo, Erick Kabendera (Tanzania), Patricia Caycho (Peru),Grevazio Zulu(Zambia) na Ebtihal Mubarak (Saudi Arabia) kazi zao ziliwaridhisha majaji na kuteuliwa kuja Umoja wa Mataifa kupitia Taasisi hiyo ya Dag Hammarskjold.

Ban Ki-moon alisema katika mazingira ya sasa ambapo dunia imekumbwa na changamoto mbalimbali, zikiwamo za kuyumba kwa uchumi wa dunia, ni rahisi kwa wananchi wanyonge na masikini kusahaulika.

Katika hafla hiyo, iliyohudhuriwa pia na mabalozi kutoka mataifa mbalimbali, Ban Ki-moon alisema Umoja wa Mataifa utaendelea kufanya kazi kwa karibu na vyombo vya habari, na kuishukuru taasisi ya Dag Hammarskjold kwa kazi nzuri ya kutoa nafasi kwa waandishi kujifunza utendaji kazi wa kila siku wa Umoja wa Mataifa.

Akisoma taarifa yake iliyowasisimua na kuwagusa wageni waalikwa katika hafla hiyo, Kabendera, alielezea changamoto mbalimbali zinazowakabili watanzania hususan katika nyanja za huduma za afya na elimu.

Kabendera aliieleza hadhara hiyo, kwamba pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na serikali katika kuboresha huduma za afya ili kinamama wajawazito wajifungue katika mazingira yaliyo salama na bora, bado uwezo wa serikali ni mdogo.

I am so sorry to all of you

I am sorry to all of you, I was not in Delhi, I went to Nainital for study tour, now I am back everythings will be under control, worry not my dear. by noor shija.

Wednesday, October 15, 2008

Shushushu wa kike anayetumia ngono akamatwa



Shushushu wa kike wa Korea Kaskazini Won Jeong-hwa, 34, ayetumia mwili wake kwa kufanya ngono na wanajeshi wa serikali ya Korea Kusini, amekamatwa Korea Kusini na kula kifungo cha miaka mitano jela. (kushoto ni ushahidi uliokusanywa na kulia ni Won Jeong-hwa.
kwa habari zaidi fungua hapa: http://shija.blog.co.in/

serikali Vietnam yamfunga jela mwandishi kwa kuandika habari za rushwa




mahakama ya Vietnam imemfunga jela miaka miwili mwandishi wa habari Nguyen Viet Chien, 56, kisa! kaandika habari za rushwa. (pichani mkewe akilia baada ya hukumu na kulia ni Viet).
Kwa habari zaidi na picha mbalimbali fungua hapa: http://shija.blog.co.in/

Ubalozi wa Uganda Ubelgiji wageuka makazi ya wavuta unga


Serikali ya Uganda imeamua kulivunjilia mbali jengo la ubalozi wake Ubelgiji kwakuwa limegeuka makazi ya wavuta unga na wahuni. jengo hilo lilinunuliwa na aliyekuwa rais wa Uganda dikteta Idi Amin Dadaa miaka kibao iliyopita. kwa habari zaidi na picha mbalimbali za jengo hilo fungua hapa: http://shija.blog.co.in/

Afrika 'tamu unapoondoka' madarakani


Mzee mzima Colin Powell akijirusha muziki wa hip-hop wakati wa tamasha la utamaduni wa Afrika lililofanyika jijini London. kwa habari motomoto kuhusu tamasha la Afrika na kujirusha kwa Powell fungua hapa: http://shija.blog.co.in/

Monday, October 13, 2008

kuachana ni ukichaa eti! wagawana nyumba



kuachana wakati mwingine huwa ni ukichaa, tazameni haya maajabu mke na mume huko Cambodia wameamua kugawana kwa kuikata katikati hii nyumba, kila mtu akachukua kipande chake, ama kweli ndoa ndoano, ikishindwa kufanya kazi inazama na mtu. (kulia ni kipisi cha nyumba).

kwa habari zaidi kuhusu hawa wanandoa bonyeza hapa http://shija.blog.co.in/ mambo yote utayapata humo. changamkia tenda mwanangu.

Saturday, October 11, 2008

Dunia ina Mambo

(hii nimeitoa kwenye blog ya Mpoki Bukuku- Mzee wa Sumo) mimi sihusiki nayo ni ya watu wa Mbeya.

(jeneza lenye maiti ya mama lasafirishwa na zawadi ndani yake)


Familia moja ilishangazwa pale walipopokea jeneza la marehemu mama yao aliyefariki nchini Marekani. Lilitumwa na mmoja ya watoto wake wa kike.
Mwili ndani ya jeneza ulikuwa umesongwa sana ndani ya jeneza kiasi kwamba uso wa marehemu ulikuwa umegusa kioo cha jeneza! Walipofungua jeneza, walikuta barua juu ya merehemu, iliyosomeka namna hii:
'Wapendwa ndugu zangu, nimeutuma mwili wa mama yetu kwa ajili ya mazishi, kwani imekuwa siku zote hamu yake kubwa kuzikwa nyumbani Ileje, katika nyumba ya ukoo.
Samahani sikuweza kuja na mwili kwani nimenyimwa likizo kwani kuna upungufu wa wafanyakazi hapa kazini mwezi huu. Ndani ya jeneza, chini ya mwili wa mama, kuna makopo 12 ya samaki wa makopo, paketi 10 za supu ya Royco na chupa 8 za jam ya maembe.
Mgawane hivi kwa jinsi mtakavyoamua nyinyi. Katika miguu ya mama kuna pea moja ya viatu vya Reebok namba 9 kwa ajili ya mtoto mkubwa wa Mwakajinga. Pia, kuna pea mbili za viatu kwa ajili ya watoto wa Mwakipesile na Ipiana , natumaini nitakuwa sijakosea namba za miguu. Nimemvalisha pia mama American T-shirts 6, kubwa kabisa ni kwa ajili ya Mwakibibi, na zinazobaki ni za watoto wake.
Hizo jeans mpya 2 ambazo mama amezivaa ni za wavulana Mwakatumbula na Mwakitobe. Hiyo Swiss watch mkono wake wa kushoto ni zawadi ya Rhoida kwa ajili ya sikukuu yake ya kutimiza miaka 21. Anti Queen, hizo heleni, mkufu na pete ambazo mama amevaa ni zako.
Hizo soksi 6 ambazo mama amevaa wagaiwe wajomba. Tafadhali mgawane kama nilivyosema na kama kuna kitu kingine mnahitaji, basi mnieleze kwani hali ya baba nayo siku hizi si nzuri sana .
Dada yenu mpenzi, Mama Mpoki

Monday, October 6, 2008

ghorofa lanyanyuliwa kwa jeki 275

Ni maajabu lakini ni kweli

Ghorofa lililojengwa kwenye eneo lililotitia na kulifanya lizame kwa futi tano na kuingia maji ndani, limenyanyuliwa kwa kutumia jeki za magari makubwa 275 kwa urefu wa futi 11. aimini usiamini mmiliki wa kampuni hiyo ana elimu ya darasa la nne na watoto wake wanne anaoshirikiano nao wana elimu ya msingi isiyozidi darasa la 10.

kwa habari za undani kuhusu jengo hilo na picha kem kem na namna walivyofanya fungua blog. http://shija.blog.co.in/ pata uhondooo!

Rais wa Pakistan alimlilia mkewe UN


Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari alitoa mpya kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa baada ya kuingia na picha ya mkewe marehemu Benazir Bhuttto aliyeuawa kwa bomu na kutaka UN iunde tume huru kufanya uchunguzi. pichani Zardari akionyesha picha yaBenazir.

habari zaidi kuhusu vituko vya Zardari ndani ya UN fungua blog. http://shija.blog.co.in/ utapata mambo kwa kirefu na upana enjoy mambooooozzzzi

'vimini Uganda stop'


vimini Uganda vinaandaliwa mpango wa kupigwa stop, baada ya waziri kudai kuwa vinasababisha ajali kwa madereva kupiga shingo kupita kiasi. kama hiki nadhani ni balaaaa.

:- Kwa habari zaidi za vimini soma http://shija.blog.co.in/ utapa mambo mengi ya kufurahisha, nenda sasa...

Saturday, October 4, 2008

this from Simon Martha Mkina:


Dear all Hope you are doing fine. I am ok.

Iam just informing you that I have been nominated a journalist of the year in Tanzania 2008 (in investigative journalism). Given a certificate and some money. Nomination was done by Media Institute of Southern Africa (Misa), USAID, Pact Tanzania and a number of journalism guru in the country.

Thanks for your cooperation.

--
Simon Martha Mkina,
Editor/Columnist/Author
Dar es Salaam
TANZANIA


0000000000000


KAMANDA WA ZAMANI WA JESHI LA RWANDA KUANZA KUJITETEA MWENYEWE JUMATATU IJAYO



Na Nicodemus Ikonko, Hirondelle,Arusha



Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Usalama Jeshini nchini Rwanda , Meja Francois-Xavier Nzuwonemeye anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kimbari katika kesi moja na maafisa wenzake watatu, Jumatatu ijayo atapanda kizimbani kuanza kujitetea mwenyewe mbele ya Mahakama ya Umoja wa Mataifa.



Mashahidi 27 wameshatoa ushahidi wa kumtetea mtuhumiwa huyo wa tatu. Wengine katika kesi hiyo ni pamoja na Makamu wake, Kapteni Innocent Sagahutu atakayefuata katika utetezi baada ya bosi wake kuhitimisha ushahidi wake.



Watuhumiwa wengine wawili ambao tayari wameshatoa utetezi wao mahakamani ni pamoja na aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Rwanda , Jenerali Augustin Bizimungu na Mnadhimu mwingine wa Jeshi la Polisi, Jenerali Augustin Ndindiliyimana.



Kwa mujibu wa Wakili Kiongozi wa mtuhumiwa Nzuwonemeye, Charles Taku kutoka Cameroon , kuna uwezekano wa kuitwa kwa mashahidi zaidi katika kesi hiyo wakiwemo wawili ambao tayari wameshaandaliwa wanaotambulika kwa majina bandia ya ‘FK’ na ‘B2’ kwa ajili ya usalama wao.



Mahakama namba II inayosikiliza kesi hiyo Septemba 22, 2008 ilitoa onyo kwa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama hiyo, Hassan Bubakar kwa kushindwa kuwapatia mawakili wa utetezi katika kesi hiyo baadhi ya nyaraka za ushahidi wa maandishi kama inavyotakiwa katika sheria iliyoanzisha mahakama hiyo.



Kwa mujibu wa Wakili Taku, tayari mwendesha mashtaka huyo ameshawapatia nyaraka tatu za ushahidi wa maandishi mawakili wa timu za utetezi kutoka katika majalada ya Kundi la zamani la Waasi nchini Rwanda (RPF).



Kesi hiyo ilianza kuunguruma mahakamani tangu Septemba, 2004



0000000000000000

Kuwe makini na Mitandao- Wanafunzi waambiwa

NA SOLOMON MWANSELE,MBEYA.

WAHITIMU wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ST.Mar's Mbeya, wametakiwa kuzitumia Intaneti kwa kujisomea zaidi, badala kuangalia picha ambazo hazina maadili mazuri kwa jamii.

Imeelezwa kuwa wanafunzi wengi hivi sasa wamekuwa na tabia ya kutumia muda mwingi intaneti wakiangalia picha hizo, hali inayochangia kuwapotosha maadili.

Changamoto hiyo imetolewa na Ofisa Tawala wa shule hizo mkoani hapa, Anuciatha Ngonyani, wakati wa mahafali ya kwanza ya kidato cha nne yaliyofanyika shuleni hapo.

Jumla ya wahitimu 48 wakiwemo wavulana tisa, walitunukiwa vyeti vyao vya kuhitimu na Ofisa Afya wa halmashauri ya jiji la Mbeya Dk.Mathias Kapizo.

Ngonyani alisema wakiwa shuleni hapo wahitimu hao wamefundishwa pia maadili mema na hivyo kuwataka kutojiingiza katika makundi ya utumiaji wa dawa za kulevya na uhuni, kwani watakuwa mfano mbaya katika jamii.

Alisema wanakwenda kwenye ulimwengu wa utandawazi ambao hivi sasa dunia ni sawa na kijiji kimoja, hivyo kuhakikisha kuwa wanajiendeleza zaidi na siyo kuishia kidato cha nne.

"Tumieni elimu mliyoipata mkiwa hapa shuleni kwa miaka minne kwa kujiendeleza zaidi kielimu huko muendako...Msipende kuzitumia Intaneti kwa kuangalia picha za ngono bali kujisomea zaidi" alisema.

Naye mgeni rasmi Dk.Kapizo alisema wahitimu hao wanatakiwa kuwa kioo kwa vijana wengine ambao hawajaweza kupata elimu kama waliyoipata yao licha ya kuwa nao wanatakiwa kujiendeleza zaidi.

Dk.Kapizo alisema:"Nidhamu ni kitu cha kwanza , pili mnatakiwa kuondoa hofu mtakapoingia chumba cha mtihani kwani mtakutana na yale yale mliyofundishwa na walimu wenu hapa shuleni".

Aliongeza kuwa hakuna mitihani inayotungwa nje ya silabasi, lakini wengi wao huwa wanafeli kutokana na kuwa na uoga wanapoingia katika chumba cha mtihani hali inayopelekea washindwe kufanya vizuri mitihani.

Kwa upande wao wahitimu hao wakisoma risala yao kwa mgeni rasmi, waliiomba serikali kutoa ruzuku kwa shule za binafsi katika baadhi ya vifaa kama vitabu na vifaa vingine vya maabara.

Walisema endapo serikali itafanya hivyo, itatoa changamoto kubwa kwa baadhi ya wanafunzi kusomamasomo ya sayansi hivyo kuongeza idadi ya wataalamu katika sekta ya afya na nyinginezo zinazotokana na masomo hayo.


0000000000000


vijimambo vya ndani ya nchi

Watoto waliokufa Tabora watajwa


* Rais Kikwete, CCM watuma rambirambi
* NSSF yatoa ubani 500,000/- kwa kila familia

Na El - hadji Yuusuf, Tabora

MAJINA ya watoto 19 waliokufa kwa kukosa hewa katika ukumbi wa disko mjini hapa, wakati wa kusherehekea sikukuu ya Idd el-Fitri juzi, yametajwa.

Wakati majina hayo yakitajwa, Rais Jakaya Kikwete, ametuma rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na wazazi wa watoto hao.

Watoto hao walianguka baada ya ukumbi wa Bubbles Night Club na Oneten Disko Teck, katika maghorofa ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kutokuwa na hewa ya kutosha, hivyo kusababisha vifo na wengine kujeruhiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa, alisema tukio hilo limeshitua wengi na kwamba limeleta hali ya fadhaa kwa wazazi na walezi.

Aliwataja watoto waliopoteza maisha katika tukio hilo kuwa Veronica Maningu, Beatrice Makelele, Jacob Gerald, Salma Hamis, Hadija Waziri, Rehema Moyo, Seleman Idd, Mrisho Seleman, Abdallah Rehani na Agatha Maningu.

Wengine waliopoteza maisha ni Paulina Emmanuel, Ramla Yenga, Mohamed Kapaya, Habiba Shaaban, Donald Kasela, Mwanahamisi Waziri, Philipo Haule, Ashura Jamal na Yassin Rashid.

Mwinyimsa aliwataja watoto waliozimia na kulazwa katika hospitali ya mkoa wa Tabora ya Kitete kwa matibabu kuwa, Sakina Ali, Daudi Chape, Shufaa Azan, Naomi Joseph, Amani Emilian, Jumanne Mashaka, Kulwa Iddi, Msimu Rehani, Bahati Hamisi na Bertha Maneno.

Wengine waliolazwa ni Asia Mohamed, Mwami Masumbuko, Shida Kassim, Kenea Masudi, Agness Kasele, Josephine Julius, Tatu Hamad na Ramadhani Idd.

Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili jana, Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tabora, Daudi Siasa alisema watoto 10 waliruhusiwa kutoka hospitalini jana, huku sita wakiendelea na matibabu.

Kutokana na tukio hilo, Mwinyimsa alisema serikali kupitia vyombo vya usalama, imeanza kuchukua hatua madhubuti baada ya kuwakamata watu waliokuwa wakipiga disko katika kumbi za Bubbles na Oneten katika jengo la NSSF yalikotokea maafa hayo.

Mbali na kukamatwa kwa watu hao, alisema serikali imeunda tume itakayofanya kazi kwa siku saba kuchunguza chanzo cha tatizo hilo.

Alisema tume hiyo itahusisha watu kutoka idara za ujenzi, Jeshi la Polisi na usalama wa taifa na inatakiwa kuwasilisha taarifa wiki ijayo.

Mwinyimsa alisema serikali itagharamia maziko ya watoto hao, na kutoa ubani wa sh. 50,000 kwa kila mzazi, ikiwa ni pamoja na kupendekeza watoto hao wazikwe mahali pamoja kwa ajili ya kuweka kumbukumbu rasmi.

Kwa mujibu wa watoto walionusurika katika ajali hiyo ndani ya kumbi hizo za starehe zilizo katika eneo moja, kulikuwa na joto kali na kulikuwa na harufu mbaya.

Walisema hali hiyo ilisababisha takriban watoto 50 kuanguka, ambapo 19 walikufa.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete ametuma rambirambi na kutuma ujumbe maalumu utakaoongoza shughuli za maziko zinazotarajiwa kufanyika mjini Tabora.

Ujumbe huo utaoongozwa na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya.

Rais alisema amepokea kwa mshituko mkubwa habari za vifo vya watoto hao na amehuzunishwa na kusikitishwa na msiba huo.

“Nimepokea kwa mshituko mkubwa, huzuni nyingi na masikitiko yasiyokuwa na kifani habari za vifo vya watoto hao wasiokuwa na hatia, ambao walikuwa wanasherehekea sikukuu ya Idd el Fitri kama tulivyokuwa tunafanya sisi sote,” alisema Rais.

Aliongeza: “Mawazo yangu yote yako kwa wazazi na wanafamilia wa watoto hao katika kipindi hiki kigumu cha huzuni, majonzi na msiba mkubwa. Tunawaombea kwa Mwenyeji Mungu waweze kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu”.

Rais Kikwete alisema ni matarajio yake kuwa, vyombo vya sheria vitachunguza kikamilifu na ipasavyo vifo vya watoto hao na kuchukua hatua zinazostahili.

Kwa upande wake, Profesa Kapuya akitoa salamu za Rais, aliuambia umati uliokusanyika katika hospitali ya Kitete mjini Tabora kwa ajili ya kuchukua miili ya marehemu hao, kuwa NSSF itatoa ubani wa sh. 500,000 kwa kila familia iliyopoteza mtoto.

Wakati huo huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa rambirambi kutokana na vifo hivyo.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Halamshauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, John Chiligati, ilisema Chama kinaungana na serikali na wazazi wa watoto waliopoteza maisha katika kipindi hiki kigumu.

Chiligati alisema ni vyema wananchi, hususan wazazi wa watoto hao kuwa na subira wakati huu, ambapo tume iliyoundwa inachunguza chanzo cha tatizo hilo


00000000000000

• Ni simanzi tu Tabora


* Baadhi ya watoto wazikwa
* Karume atuma rambirambi

Na El - hadji Yuusuf, Tabora
WAZIRI wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, jana aliwaongoza mamia ya wakazi wa Tabora, katika mazishi ya watoto 19 waliokufa kwa kukosa hewa wakiwa kwenye kumbi za disko kusherehekea sikukuu ya Idd el Fitri.

Mazishi ya watoto hao yalifanyika kwenye maeneo mbalimbali, Profesa Kapuya, ambaye alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete, alihudhuria ya watoto wanne.

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi ya watoto hao ni Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki, mkoani humu na mkewe, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margaret Sitta, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu.

Wengine ni Mkuu wa mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau. Maafa hayo yalitokea kwenye jengo la shirika hilo.

Profesa Kapuya, ambaye ni Mbunge wa Urambo Magharibi, alihudhuria mazishi ya watoto hao, waliozikwa katika maeneo ya Ng’ambo na Rufita.

Spika Sitta alihudhuria kwenye mazishi ya watoto wawili yaliyofanyika eneo jirani na uwanja Ali Hassan Mwinyi.

Watoto hao walikubwa na maafa hayo Jumatano wiki hii, wakiwa disko kwenye kumbi za Bubbles Night Club na Oneten Disco Theque.

Watoto 16 walijeruhiwa, ambapo hadi jana wanne bado walikuwa wakiendelea na matibabu kwenye hospitali ya mkoa ya Kitete.

Kwa mujibu wa Mwinyimsa, hali za watoto hao zinaendelea vizuri, licha ya kukaa muda mrefu bila ya kupata fahamu.

Aliwashukuru wananchi kwa kuwa watulivu tangu mkasa huo ulipotokea na kwa ushirikiano waliouonyesha katika kipindi hiki kigumu.

Akizungumzia kuhusu tume aliyoiunda kuchunguza tukio hilo, alisema inaanza kazi leo.

Alisema moja ya mambo ambayo yanatarajiwa kupatiwa ufumbuzi na tume hiyo ni kujua kama wafanyabiashara wa kumbi hizo walifuata sheria na taratibu, kama kumbi hizo zilikuwa na nafasi ya kutosha na vifaa vya tahadhari.

Mwinyimsa alisema tume hiyo itawahoji watu muhimu na wale ambao wataonekana kuwa na uwezo wa kutambua kilichojiri katika ukumbi huo, wakiwemo watoto walionusurika.

Aliwataja watu wengine ambao tume hiyo inatarajiwa kuwahoji kuwa, wamiliki wa kumbi hizo, mameneja, wazuia fujo katika kumbi hizo na watu wengine watakaojitokeza, ambao wanaweza kuipa ushirikiano tume kufanyakazi vizuri.

Mwinyimsa alisema polisi inawashikilia Shashikant Patel, mkurugenzi wa Bubbles Night Club na meneja wake Vituko Salala.

Wengine ni Mkurugenzi wa Oneten Disco Theque, Projestus Fidelis ‘Porojo’ na meneja wake, Jaffar Rashid.

Alisema walinzi wa milangoni waliokimbia baada ya tukio hilo, wanaendelea kusakwa na polisi.

Kwa mujibu wa Mwinyimsa, serikali itachukua hatua dhidi ya watakaobainika kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kusababisha tukio hilo.

Katika hatua nyingine, Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, ametuma rambirambi kwa wananchi wa Tabora kutokana na vifo hivyo.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Rais Karume alieleza kushtushwa na vifo hivyo, vilivyohusisha watoto wadogo wasio na hatia.

Alisema taifa limepata hasara kuwapoteza watoto, ambao ni matumaini ya wazazi na taifa.

Katika hatua nyingine, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, imetuma rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa watoto waliofariki dunia katika tukio hilo.

Rambirambi hizo zilitolewa jana na wizara kupitia Msemaji wake Erasto Ching'oro, aliyesema wizara imepokea kwa masikitiko makubwa na kwamba msiba huo ni wa taifa.

Wakati huo huo, Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), kimetoa pole kwa familia za watoto hao, na kuitaka serikali ichukue hatua kuhakikisha viwanja vya michezo na burudani vilivyoporwa na matajiri vinarejeshwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho, Ananilea Nkya, alisema wamekuwa wakifuatilia na kubaini katika miaka ya hivi karibuni maeneo mengi yaliyokuwa yametengwa kwa ajili ya michezo yamegeuzwa viwanda vidogo, gereji, baa, migahawa, maduka, hoteli na vituo vya mafuta.


000000000000000

• Uchunguzi makini ufanyike vifo vya watoto Tabora


MAONI……

MARA kwa mara, wakati wa maadhimisho ya sikukuu, limekuwa jambo la kawaida kuripotiwa watu kufa katika ajali za barabarani na wengine kupigwa kutokana na ugomvi, hususan kwenye maeneo ya starehe.

Katika maadhimisho ya sikukuu ya Idd el-Fitri yaliyofikia kilele juzi, pia kumeripotiwa kutokea mambo mbalimbali katika sehemu mbalimbali hapa nchini yakiwemo ya watu kupoteza maisha.

Licha ya kuwepo mambo mengi, kubwa zaidi ni la kupoteza maisha kwa watoto 19 kwenye ukumbi wa disko huko Tabora. Hayo ni maafa makubwa na ya kutisha.

Imeripotiwa kuwa watoto hao, wanane wakiwa wavulana na 11 wasichana, walikufa kutokana na kukosa hewa katika ukumbi wa disko wa Bubbles,na oneten,zilizoko katika jengo linalomilikiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa, watoto waliokufa wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka saba na 18. Wengine 16 walilazwa katika hospitali ya mkoa, watatu hali zao zikiwa mbaya.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa watoto hao walijaa kupita uwezo wa ukumbi, jambo lililosababisha mzunguko wa hewa kuwa mdogo.

Wakurugenzi kadhaa wa ukumbi huo imeelezwa wanashikiliwa na polisi kwa kuhojiwa kuhusu tukio hilo la kusikitisha.

Mwinyimsa alisema kamati imeundwa kuchunguza tukio hilo, ikihusisha maofisa kutoka Polisi, Usalama wa Taifa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Tukio hilo linaonyesha wazi kwamba, wenye ukumbi hawakuwa makini katika kusimamia shughuli hiyo.

Ni jambo lililo dhahiri kwamba walijali zaidi maslahi binafsi, badala ya afya za walioingia kwenye ukumbi huo.

Katika msongamano huo, licha ya waliopoteza maisha, kuna uwezekano mkubwa wa baadhi ya watoto hao kuambukizwa maradhi yanayoenezwa kwa njia ya hewa.

Wakati tunaungana na familia za watoto waliopoteza maisha, tungependa kushauri mambo kadhaa juu ya hatua ambazo tunadhani zinafaa kuchukuliwa.

Kwanza, tume iliyoundwa kuchunguza maafa hayo ifanye kazi kikamilifu na umakini mkubwa, ili matokeo yatoe picha halisi ya chanzo chake.

Pili, kwa kuwa uchunguzi unahusisha vyombo vya dola basi endapo itabainika kuwepo uzembe kwa upande wowote hatua stahiki zichukuliwe kwa waliohusika.

Tunasema haya kwa sababu hatuamini kwamba watoto wanaweza kujaa kwenye ukumbi kiasi cha kukosa hewa bila tahadhari yoyote ya madhara ambayo yangeweza kutokea.

Hivyo katika uchunguzi huo, ni vyema jengo hilo likachunguzwa ujenzi wake, na ikibainika haukuzingatia taratibu na halifai kwa shughuli za disco wahusika wawajibishwe.

Kwa kifupi mamlaka husika zinapaswa kuchukua hatua madhubuti kwa wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo, ili lisijirudie katika siku zijazo.


00000000000000000

Mgombea ugavana amtwanga mwandishi


BANGKOK, Thailand

MMOJA wa wagombea ugavana wa jiji la Bangkok juzi alimshambulia kwa ngumi na mateke mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni kwa madai ya kukerwa na maswali magumu.

Mgombea ugavana huyo, Chuvit Kamolvisit alikuwa akiulizwa na mwandishi huyo, huku mahojiano hayo yakirushwa moja kwa moja.
Hata hivyo, mgombea huyo aliomba radhi, akisema alipandwa na ghadhabu baada ya kuona kuwa maswali ya mwandishi huyo, Visam Dilokwanich, yanalenga kumuumbua ili anyimwe kura kwenye uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika kesho.

“Nakiri nilifanya hivyo. Sikuvumilia kwa kuona ananiumbua moja kwa moja kupitia televisheni,” alisema Chuvit, mtu wa miraba minne aliyewahi kumiliki baa kadhaa jijini Bangkok, zenye wahudumu wanaovalia vivazi vya nusu uchi.

“Nilichofanya ni uhalifu, na ni haki kwangu kulipa faini kwa kumdunda kwa ngumi na mateke,” aliongeza Chuvit, ambaye hana nafasi kubwa ya kushinda kwenye uchaguzi huo.
Mwanahabari huyo alifungua kesi polisi, akisema Chuviot alionekana kama jambazi.

“Alikasirika sana nilipomwambia kwamba alichokuwa akisema katika mahojiano hayo yalikuwa tofauti sana na anachokisema akiwa sehemu nyingine,” alieleza Visarn, akiwaonyesha wanahabari wenzake majeraha aliyopata shingoni na kichwani baada ya kipigo.


00000000000000

• Ndege tano zaporwa Mexico


MEXICO CITY, Mexico

WATU wenye silaha juzi walipora ndege tano ndogo kutoka kwenye uwanja binafsi, katika mji wa Kaskazini Magharibi mwa Mexico wa Sinaloa, baada ya kumzidi nguvu polisi.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, waporaji hao, wanaokadiriwa kufikia 20, walivamia uwanja huo mdogo wa ndege alfajiri, wakamnyang’anya polisi bunduki, wakamfunga kamba, wakajaza mafuta katika ndege hizo, na hatimaye wakaruka.

Msemaji wa kikosi cha polisi kinachopambana na mtandao wa kihalifu, Emma Quiroz alisema kuwa haikufahamika iwapo kuna uhusiano kati ya waporaji hao na genge linalojihusisha na dawa za kulevya aina ya ‘cocaine’.

Kundi hilo kwa kawaida hutumia ndege ndogo kusafirisha dawa hizo Kaskazini mwa Mexico hadi mpakani na Marekani.
Alieleza kuwa polisi wanachunguza iwapo uporaji huo ulifanikishwa kwa msaada wa baadhi ya maofisa serikalini.

Taarifa ilieleza kuwa vyombo vya usalama vilikuwa vikifuatilia kujua wapi ndege hizo zimepelekwa, na pia kuwakamata waporaji. Alisema ziliporwa eneo la kufanyia matengenezo kwenye uwanja huo unaomilikiwa na kampuni ya kunyunyizia dawa mazao ya kilimo mjini Navolato.

Jeshi lilizisimamisha ndeghe hizo kutoa huduma mapema mwaka huu, kwa maelezo kuwa hazikuwa katika hali nzuri ya kukidhi usalama wa anga.

Jeshi la ulinzi, ambalo pia linashiriki kukabiliana na genge la dawa za kulevya nchini Mexico, na hasa kwenye majimbo ya Kaskazini, limeshakamata ndege ndogo 245, zikiwemo helikopta, tangu Novemba, mwaka jana.

Sinaloa ni moja ya majimbo ambako magenge yanayojihusisha na biashara ya dawa za kulevya yanakabiliana vikali na jeshi, ambalo kwa mwaka huu pekee limeua watu wapatao 3,000. Ndege ndogo hutumiwa kihalali kunyunyizia dawa mazao mashambani, na vilevile kuteketeza kilimo cha bangi.


00000000000000